Baada ya baadhi ya watu kumshtumu, muigizaji wa Bongo movie, Wastara kuwa asumbuliwi na mguu ila anataka ela kwa ajili ya mambo yake binafsi na si kujitubu mguu, msanii huyo awajia juu watu hao.
Wastara amesema kuwa anashangaza na watu hao wanaosambaza habari hizo kwani yeye anasumbuliwa kweli na mguu na anahitaji kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya mguu huo.
Muigizaji huyo amewajibu watu hao baada ya kumtuhumu kuwa tapeli kwani hana ugonjwa unaomsumbua bali anataka pesa ya kujitibu.
Wastara amesema kabla ya kuomba michango alijitahidi sana kujitafutia mwenyewe hiyo pesa kwani hakutaka pesa ya mtu mwengine ije imsaidie, kwani alijiona anakuwa mzigo kwa jamii.
Wastara amesema alishajaribu kujiingiza kwenye biashara ambazo amedai hazina faida, mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza vitu vya ndani, jambo ambalo msanii mwenzake Steve Nyerere alimkataza na kumshauri aweke wazi matatizo yake iili watu wamsaidie.