Muigizaji wa filamu, Wastara Juma amemuomba pesa ya matibabu Rais John Pombe Magufuli baada ya kutapeliwa na kampuni moja ya simu ambayo ilimteua kama balozi wa bidhaa zao.
Muigizaji huyo amedai ametapeliwa zaidi ya tsh milioni 80 na kampuni hiyo ya simu pesa ambayo amedai alikuwa anajichanga kwaajili ya matibabu ya mguu wake nchini India.
Muigizaji huyo amesema kuwa aliteuliwa na kampuni ya simu ya wachina KZG kama balozi laini badala yake wakamtepeli milioni 80 alizokuwa anataka kutumia kwa matibabu ya mguu wake nchini India.
Wastara ameendelea kusema kuwa jinsi nahitajika kurudi hosptal india Sifael hosptal tokea tal 12/02/2017 ambapo nilitakiwa nifanye matibabu kwa mda wa miaka 2 chini ya uwangilizi wa hosptal hiyo kabla ya kufanya maamuzi ya kufanyiwa operetion ya mgongo hivyo kila tal 12/ 2 natakiwa kurudi hosptal nimejitahidi kupambana peke yangu kutafuta pesa ya kunirudisha hosptal nimeshindwa
Pia ameongeza kwa kusema kuwa Mwezi wa 3 mwaka jana ameenda nchini sweden kufanya filamu nimerudi mikono mitupu mwezi wa 4 nimedai pesa yangu steps tumeishia kwenda mahakamani bila kulipwa nilivyokuwa natarajia tokea hapo chchote ninachofanya kinachohusu pesa lazima tuishie polisi au mahakamani silipwi vile tunavyokubaliana na baya zaidi ninaofanya nao kazi awajui kuwa tokea nimerudi nchini toka sweden anahaha kutafuta pesa ya matibabu.