Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu ambavyo anavijutia kwenye maisha yake ni kufunga ndoa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.
Wastara amesema anajutia uamuzi huo kwani hakumjua vizuri kabla ya kukubali kufunga naye ndoa amesema kwamba alikubali kufunga ndoa na mwanaume huyo pasipo kumjua ni mtu wa aina gani.
Wastara aliolewa na Mbunge huyo kama mke wa pili mwaka jana ambapo ndoa hiyo ilidumu kwa miezi kadhaa na baadae kuvunjika kwa kile alichodai Ahadi zake hazikutimizwa kwenye ndoa hiyo.
Pia Wastara amedai kuwa sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.
Hivi karibuni muigizaji huyo aliwasili nchini akitokea nchini India alipokuwa anatibiwa mguu wake uliokuwa unamsumbua baada ya kupata ajali.