Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amedai kuwa ameanza kufanya muziki na tayari ameanza kuandaa albam yake.

Wastara amesema kuwa ameamua kujiingiza kwenye muziki kutokana na kuwa na kipaji cha kuimba licha ya kuigiza.

Muigizaji huyo ameanza kufanya video yake ya kwanza aliyowaimbia wanawake na kusema kuwa tayari ameshakamilisha albam yake ambayo ndani ya mwezi huu atakuwa ame’shoot’ video 3 kwa mpigo, na albam itakamilika mwezi Juni mwaka huu.

Pia amesema show yake ya kwanza ataifanyia Sweden tarehe 18 mwezi huu kwenye kongamano la wanawake kutoka bara la Afrika ambapo yeye amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania.

Muigizaji huyo amejiunga na waigizaji wenzake Shilole na Snura ambao wameingia kwenye kuimba licha ya kuwa waigizaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *