Muigizaji wa Bongo movie, Wastara Juma amefunguka na kudai kuwa michango anayochangiwa na wasamaria wema kwa ajili ya matibabu ya mguu wake inaibiwa na watu wasiokuwa wahaminifu kwake.
Wastara aliomba wasamaria mema wamsaidie kupata pesa ambayo itamsaidia kwenda kutibiwa mguu wake ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Wastara pia aliiomba serikali imsaidie kupata matibabu zaidi kwani amedai maumivu makubwa zaidi aliyapata wakati wa kampeni.
Wastara alianza kusumbuliwa na mguu miaka kadhaa iliyopita baada ya kupata ajali ya gari iliyopelekea kukatwa mguu mmoja na hivyo kupelekea ukilema wa mguu mmoja.
Baada ya kuomba msaada huo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari Wastara alianza kupata michango kutoka kwa watu mbali mbali lakini kwenye mahojiano na Global publishers Wastara amedai kuwa amekuwa akidhulumiwa pesa zake bila kuelewa zinaenda wapi
Lakini pia Wastara amesema kuwa anasikitishwa na watu Wanaosema yeye kageuza michango ya watu mtaji kwani sio kweli na mguu wake umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.