Aliyekuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi katika Jimbo la Bunda Mjini mwaka 2015, Lucy Msoffe amekiri kufanya makosa ya kuandika idadi ya wapigakura wakati wa kutangaza mshindi wa nafasi ya ubunge.

Akizungumza katika mahojiano na wakili wa upande wa mjibu maombi wa pili, Tundu Lissu katika kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo hilo inayoendelea mjini Musoma.

Msimamizi huyo alisema siku ya kutangaza matokeo alikuwa hajalala tangu tarehe 24 usiku hadi muda ambao alitangaza matokeo saa 11:11 jioni.

Amesema kutokana na uchovu mwingi ndiyo maana akawa anakosea kuandika idadi ya wapigakura mara mbili mfululizo wakati wa kutangaza mshindi.

Kesi hiyo ni ya kupinga matekeo yaliyompa ushindi mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (CHADEMA) imefunguliwa na aliyekuwa mgombea mwenzake katika jimbo hilo Steven Wasira (CCM).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *