Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wasira amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa mambo manne.
Moja ya mambo ambayo Wasira amesema ni kwamba mbunge huyo wa Chadema hana heshima kwa viongozi wakuu wa nchi.
Wasira alisema hayo baada ya Lissu kudai kuwa alinusurika kupigwa na kada huyo wa CCM wakati wa vikao vya Bunge mjini Dodoma, habari ambayo ilichapishwa jana na Mwananchi.
Akijibu tuhuma hizo, Wasira (pichani) alisema Lissu anaongea kama vile hayuko sawasawa kwa sababu yote aliyoyasema ni uongo, hajui yalitokea wapi na hajui sababu zake.
Wasira alisema hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kumtukana Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, lakini alimshangaa Lissu alipothubutu kufanya hivyo wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.
Alisema Lissu pia alimtuhumu mambo ya uongo Mwalimu Nyerere kwa kudai alighushi saini ya mwasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeid Amani Karume kwenye hati ya Muungano. “Hata wapinzani wenzake walimshangaa.