Wasichana 21 waliokuwa miongoni mwa wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram eneo la Chibok nchini Nigeria wameachiwa huru.

Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amethibitisha kuachiliwa huru kwa wasichana hao.

Bw Mallam Garba Shehu ameandika kwenye Twitter: “Imethibitishwa kwamba wasichana 21 wa Chibok wameachiliwa na kwa sasa wamo mikononi mwa Idara ya Masuala ya Serikali.”

Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.

Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *