Wasichana 21 waliotekwa na kundi la Boko Haram miaka miwili iliyopita, ambao waliachiliwa huru jana, wamekutana na makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo.

Bw Osinbajo amesema wasichana wote wamo buheri wa afya. Rais Muhammadu Buhari yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani.

Amesema waliachiliwa kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana, ambapo wafungwa wanne wa kundi la Boko Haram waliachiliwa huru na serikali.

Lakini serikali imekanusha madai hayo kwamba makamanda wane wa Boko Haram waliachiliwa huru ndipo kundi hilo likubali kuwaachilia huru wasichana hao.

Kundi hilo liliwateka zaidi ya wasichana 250 kutoka kwenye shule ya Chibok Aprili mwaka 2014, kisa kilichoshutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.

Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni miongoni mwa walioshiriki kampeni ya kutetea kuachiliwa huru kwa wasichana hao iliyokuwa na kitambulisha mada #BringBackOurGirls.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *