Wadau  wa tasnia ya filamu Tanzania, wametaka mabasi kulipa Sh50 kwa kila abiria aliyepanda pale wanapoonyesha kazi zao katika usafiri huo.

Wametoa mapendekezo hayo, Septemba 17, 2021 katika kikao chao na  Taasisi ya Hakimiliki (Cosota), kilichofanyika ukumbi wa Costech.

Pamoja na mambo mengine katika kikao hiko, moja ya mada iliyojadaliwa na kuwa na maoni mengi ni suala la ukusanyaji mirabaha ya kazi za famu katika mabasi ambalo linatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akielezea  utekelezaji wa suala hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare amesema kiwango kilichowekwa kwa mabasi na kukubaliana na wamiliki wake ni  Sh50,000 mabasi ambayo ni daraja la juu (luxury), daraja la kati (Semi Luxury) Sh30,000 na mabasi yanayofanya safari za ndani mikoa Sh20,000.

Kiasi hicho ambacho kitatozwa kwa mwaka, Doreen amesema wamekipitisha kama moja ya njia ya kuanzia kuwa kazi hizo zinapotumika kwenye mabasi zinapaswa kulipwa na kuongeza kuwa wataziboresha kadri watakavyopata maoni kutoka kwa wasanii wenyewe.

Wakichangia jambo hilo  kwa nyakati tofauti, wadau hao akiwemo Silvanus Mumba, amesema kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na gharama wanazotumia kuziandaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *