Baadhi ya wasanii nchini wamevunja ukimya kuelekea kwenye fainali ya tuzo za filamu itakayofanyika Desemba 4 mwwaka huu.

Tamasha la tuzo za filamu lililoandaliwa na Serikali kupitia bodi ya filamu nchini litashindanisha filamu 112 zitakazochuana kwenye vipengere 30 tofauti.

Vipengere hivyo ni tamthilia bora, filamu bora ndefu, muigizaji bora wa kike na wa kiume, muongozaji bora, muigizaji bora wa kike na wa kiume, muswada bora, muongozaji bora wa kike na wa kiume, muigizaji bora wa kike na wa kiume chaguo la Watanzania na filamu bora ya makala, filamu bora fupi na tuzo ya heshima.

Vipengere vingine ni filamu bora katika animesheni, sauti, uhariri, muziki, mavazi, haiba, mandhari, usanifu, mapambo, ucheshi, mchekeshaji bora, muigizaji bora chipukizi wa kike na wakiume na vipengere vingine.

Wasanii baadhi wamesema uwepo wa tuzo hizo utaongeza hamasa kwa wasanii kufanya kazi bora zaidi.

“Tofauti na mwanzo tulikuwa tunafanya filamu tu basi umemaliza, lakini sasa tnafanya tukitegemea mwisho wa mwaka kuna kuwania tuzo, bahati nzuri tumeambiwa tuzo hizi zitakuwa ni endelevu,” amesema Suzan Lewis “Natasha”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *