Wasanii wa Bongo Movie chini ya lebo WCB wamekuwa wakivuna “views” ama watazamaji wengi katika mtandao wa YouTube mara tu wanapoachia video zao mpya.

Wasanii hao wamekuwa wakifikisha watazamaji millioni 1 ndani ya saa 24 au hata kabla ya saa 24 kufika na kufanya wasanii hao kuwa wasanii ambao kazi zao zinafuatiliwa sana katika mtandao wa YouTube.

Lakini sasa hali hiyo imekuwa tofauti kidogo kwa wasanii wa wawili wa lebo hiyo, Rayvanny na Mbosso kushindwa kufikisha watazamaji millioni 1 katika video zao za YouTube walizoachia hivi karibuni hata baada ya saa 72 kupita.

Hapo mwanzo Rayvanny alikuwa akifikisha watazamaji millioni 1 katika video zake kama Pepeta, Tetema na I love you lakini hivi sasa yake ya “Chawa” ambayo aliiachia siku nne zilizopita imetazamwa mara 975k tu, pia,

Mbosso amefikisha watazamaji 850k katika video yake mpya ya “Your Love” ndani wa wiki moja, tofauti na hali ipokuwa hapo mwanzo katika nyimbo zake kama Haijakaa Sawa, Sina Nyota na Hodari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *