Wasanii 10 wa Bongo Fleva wanaouza zaidi kwenye mitandao kutokana na ubora wao wa muziki hapa nchini.

 

1; DIAMOND PLATNUMZ

 

Anashika namba moja akiwa na zaidi ya streams na views bilioni 1.6 ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya msanii yeyote Bongo; maana yake ni kwamba ukizigeuza kuwa pesa, basi ni mabilioni ya shilingi.

 

2; RAYVANNY

 

Rayvanny ana zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 664 ambazo hizo zote ni mkwanja mzito.

 

3; HARMONIZE

 

Yeye anashika nafasi ya tatu akiwa na zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 661 wanaomuingizia mamilioni ya pesa.

 

4; MBOSSO

 

Anashika nafasi ya nne kulingana idadi ya watazamaji na wasikilizaji wengi kupitia mitandao hiyo mikubwa minne ya kimataifa. Mbosso ana zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 440 ambao wanampa pesa za kutosha.

 

5; ZUCHU

 

Yeye ana zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 324 wanaomfanya kuwa mrembo kinara anayeingiza mkwanja mrefu kupitia mauzo ya muziki wake kwenye mitandao hiyo.

 

6; Alikikiba

 

kiba ana zaidi ya watazamaji na wasikilizaji milioni 184 wanamng’arisha kwa mkwanja wa kutosha.

 

7; LAVA LAVA

 

Yeye anakimbiza akiwa nafasi ya saba na zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 171.

 

8; NANDY

 

Nandy amefanikiwa zaidi kwenye Bongo Fleva kwa muda mfupi kutokana na ladha na kipaji chake cha pekee kisha kutamba na tamasha lake mwenyewe la Nandy Festival. Nandy ana wasikilizaji na watazamaji zaidi ya milioni 168 ndani na nje ya Bongo.

 

9; DARASSA

 

Anashika nafasi ya tisa akiwa ni kati ya wasanii wachache wa Hip Hop Bongo waliosikilizwa zaidi.

Darassa ana zaidi ya wasikilizaji na watazamaji milioni 84 kwenye mitandao hiyo pekee.

 

10; MARIOO

 

Anafunga nafasi ya mwisho kwa kuzingatia watazamaji na wasikilizaji katika mitandao hiyo minne mikubwa ambayo tumeifanyia uchambuzi. Marioo ana zaidi ya watazamaji na wasikilizaji milioni 72 wanaompa jeuri ya pesa za kutosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *