Taasisi ya Wasafi Media imetoa shilingi milioni 15 Tsh. kwa ofisi ya Bakwata ya Mkoa wa Dodoma Kwa ajili ya kuendeleza vituo vya mafunzo ya kiislam (Madrasa).

Akizungumza Dodoma kwenye tukio la la fadhira za Ramadhani Iftar lililofanyika katika viwanja vya Bunge Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi, Diamond Platnumz amesema fedha hizo zitakwenda kusaidia kununua vitabu vya kusomea, Busati na mikeka kwa ajili ya kuswalia

Nasibu amekabidhi fedha hizo Kwa Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson ambapo Spika amemkabidhi sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu.

Diamond amesema kuwa hiyo ni mwanzo na wataendelea kutoa kwa wahitaji maalum ili kuweza kuwasaidia pale inapohitajika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *