Kituo cha runinga cha ‘Wasafi Tv’ kimerejea rasmi hewani baada ya kufungiwa kurusha matangazo na mamlaka ya mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ miezi miwili iliyopita.
Wasafi ilifungiwa kurusha matangazo kwa miezi sita(6), Januari 05 2021, baada ya kukiuka kanuni za urushaji wa matangazo kwa kurusha maudhui yenye utupu.
Hata hivyo Februari 04 2021 Wasafi ilipunguziwa kiwango cha adhabu na TCRA kutoka miezi sita mpaka miezi miwili kufikia Februari 28 2021.
Wasafi Tv ilipunguziwa adhabu baada ya tafakari ya TCRA, hiyo ni baada ya kituo hicho kuwasilisha maombi na vielelezo zaidi kikiomba mamlaka kupitia upya uamuzi uliotolewa.
Baada ya uamuzi kupitiwa, Wasafi TV ilitakiwa kuendelea kutumikia adhabu hadi Februari 28, 2021, huku ikipewa muongozo wa kuendelea kuzingatia masharti ya leseni.