Mwanasheria mkuu wa Malaysia amesema wanawake wawili wanaodaiwa kumuua ndugu wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un watashtakiwa kwa makosa ya mauaji.

Wawili hao, raia wa Indonesia na Vietnam wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa mauji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.

Malaysia imesema kuwa Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu aina ya , VX, ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.

Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uanjwa wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.

Hatahivyo hakuna hatua iliochukuliwa kuhusiana na kumshataki raia wa Korea Kaskazini ambaye pia anazuiliwa kwa muaji hayo.

Washukiwa hao ni pamoja na afisa mkuu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur pamoja na mfanyikazi mmoja wa kampuni ya ndege ya taifa hilo.

Korea Kusini inaamini kwamba washukiwa wanne ni wapelelezi wa Korea Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *