Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa watu watakaosambaza takwimu mbalimbali za kupikwa kukamatwa na kuwekwa ndani na baadaye kupelekwa mahakamani.

Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hala watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.

Mbali na hilo Rais Magufuli ameagiza watu ambao watatoa taarifa zozote ambazo zipo kinyume na takwimu walizonazo watu wa takwimu wafikishwe mahakamani …..”Mimi ningekuwa hakimu watu wa namna hiyo wangepewa adhabu zote mbili kulipa faini na kufungwa”

“Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uchumi umeshuka.

“wanaosema vyuma vimebana, vitabana tu kwa wale waliokuwa wamezoea fedha za bure bure, na vitaedelea kubana kweli kweli Lakini kwa wale wanaochapa kazi, kwa mfano wakazi wa Lindi na Mtwara, walikuwa wanauza korosho saa nyingine kwa bei ya chini mpaka elfu 2 kwa kilo, sasa elfu 4 kwa kilo.

“Wale vyuma haviwezi vikabana, wale vyuma vimeachia, nasikia wanaamua hata mbuzi kuzinywesha bia, kule vyuma vimefungua., hivyo wapuuzieni watu wanaowadanganya vyuma vimekaza”, amesema Rais Magufuli.

Mbali na hilo Magufuli amewataka wananchi na taasisi mbalimbali wakitaka takwimu yoyote ile waende ofisi ya Takwimu na wasithubutu kutoa takwimu ambazo zinapingana na zile zilizopo ofisi ya takwimu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *