Wanafunzi 29 na walimu wao wamefariki dunia baada ya basi la wanafunzi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.
Wanafunzi hao ni wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & Primary School English Medium iliyopo Arusha, walikuwa wakienda karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu.
Wanafunzi wanne(4) pekee ndiyo wanasadikiwa kuwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeru wa ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha na kusema atatoa taarifa kama ajali hiyo imesababisha madhara akifika eneo la tukio.
Habari kutoka Hospital ya Lutheran Karatu maiti zilizopokelewa hapo hospitali ni maiti 32 miongoni mwao walimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wavulana ni 11 na wasichana 18 nakufanya jumla hiyo ya maiti 32.