Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametia saini muswada inayowaruhusu wakopeshaji kutumia vifaa vya nyumbani mimea na mifugo ili kujipatia mikopo.

Sheria hiyo kwa jina Movable Property Security Acto 2017 inatotoa fursa kwa kuanzishwa kwa sajili ya kwa mali hiyo ambazo benki zinaweza kutumia kuthibitisha umiliki dhamana yake.

Sheria hiyo mpya inalenga kuwasaidia wateja wa benki wasio na magari na vyeti vya umiliki wa gari ama hata ardhi kupata mkopo ambapo sheria hiyo inakuza uthabiti na uhakika kwa kutoa dhamana ya mali .

Benki zimekuwa zikikataa kutumia mali inayoweza kuhamishwa kama dhamana ya mkopo kutokana na ukosefu wa data ambayo wanaweza kutumia ili kudai mali hiyo.wanaweza kutumika kupata mkopo katika benki Kenya

Uidhinishaji wa sheria hiyo huenda ikaigharimu serikali kwa kuwa ni sharti iweke sheria kama vile thamani ya chini ya mali inayoweza kutumika kama dhamana.

Sheria hiyo pia itabainisha ni mali gani ambayo inafaa kutumika kama dhamana kwa anayetaka mkopo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *