Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa akijafurahi jinsi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyomtaja mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwenye orodha ya watuhumiwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya bila kufuata utaratibu.

CHADEMA wamesema kuwa wao hawapingi kutajwa kwa kiongozi huyo kwenye orodha hiyo ila wanapinga utaratibu alioutumia Makonda kutaja jina la kuingozi huyo wa juu wa chama hicho ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni.

Kiongozi mmoja wa chama hicho amesema kuwa kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani.

Pia ameongeza pia  “Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita,.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametaja orodha ya watu wanaohujihusisha na biashara ya kulevya ambapo amewataja Freeman Mbowe, Yusuf Manji, Idd Azzan Mchungaji Gwajima na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *