Wakili maarufu nchini, Peter Kibatala amejitolea kumtetea mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego aliyekamatwa jana mkoani Morogoro kutokana na kuimba wimbo unaokosoa Serikali iliyopo madarakani.

Nay wa Mitego jana amekamatwa mkoani Morogoro na amesafirishwa hadi jijini Dar es Salaam na kufikishwa Central kutokana kosa hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakili Kibatala ameandika kuwa “Nay wa Mitego amefikishwa Central Police Station, Dar es Salaam yuko salama na imara amekula pia. Kwa kuwa amefika jioni sana; hakuna kinachoweza kufanyika leo Wakili Faraji Mangula alifika pale, na kesho tutapigana afikishwe Mahakamani au apewe dhamana.

kibatala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *