Wake wa viongozi Mama Janeth Magufuli pamoja na mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa wamewataka Watanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu nchini.

Wamewataka watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.

Wake hao wa viongozi wamesema hayo jana walipotembelea makazi ya wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni, mkoani Singida.

Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage.

Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo hiko kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi na kinawafikia kama kilivyopangwa.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *