Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Wakazi ameandika ujumbe wa kushinikiza Mamlaka husika kumfungulia msanii mwenzake Gigy Money ambaye amefungukiwa na Basata.
Wakazi ameandika haya kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram “FREE GIGY MONEY akitaka msanii huyo afunguliwe na afanya muziki.
Kuna Wasanii tena wakubwa wanafanya mambo ya ajabu, kinyume na Maadili tuliyoyazoea, wanaachwa HURU, alafu GIGY MONEY ambae alitumia “Ubunifu wa Mavazi” akashutumiwa yupo UCHI na kufungiwa Miezi 6.
Double Standards za kwenye maamuzi kea kweli zina kera na zinaumiza wengi sana. Tunafumbia macho baadhi ya mambo, na kuwaangushia jumba bovu wengine ambao hata hatia hawana.
Mh Rais Hassan amefungulia VYOMBO VYA HABARI, ila pia nadhani Watendaji wake nao inabidi wafungulie Wasanii ambao walikatazwa kufanya Sanaa kimakosa kama Gigy.
Pia amesema kuwa alafu kisha tukae Vikao vya kufanya Maboresho ya Kanuni, Sheria, Sera na mengineyo ili SANAA iende na Wakati, ikue ki-UBUNIFU na pia IWANUFAISHE wote wanaoifanya ili nao waweze kusaidia familia zao, na pia kulijenga Taifa (Kupitia Kodi).