Mwanamuziki wa Hip Hop, Wakazi amezikemea vikali sheria na kanuni zilizopitishwa na basata kwa kile alichodai kuwa ni uhalifu wa sanaa na ubunifu.

 

Wakazi kupitia taarifa hii iliyothibitishwa kutoka kwenye ukurasa wake wa instagram ameoliomba bunge pia liingilie kati na kutunga upya sheria hizo kandamizi.

 

“Viongozi wasio na Maono wanatuongoza kwenye giza kama sio shimoni, pia uoga wao wa kukusolewa au kuona Wasanii wakiwakosoa kunawafanya wachukue hatua ya kuwafumba midomo, na wengine wapo tayari hata kuwadhuru baadhi ili uwe mfano kwa wote.

 

Na mara nyingi hufanya hivyo kwa maslahi ya Kisiasa kwaajili ya Watu fulani ingawa kisingizio utakachopewa ni Maadili”.

Sasa pengine nilichosema nilionekana nabwabwaja, ila BASATA wamefanya just that… Na finally naona hadi Wasanii ambao huwaga wanakaa kimya nao wameamua kufunguka. Sasa basi tuungane kweli tuwe Sauti Moja, na tupiganie haki zetu za kuwa Wasanii, kuwa Kioo Cha Jamii, kuwa na UHURU wa kujieleza, na kufanya BIASHARA ya Tasnia ya Ubunifu kwa kuongozwa na Sheria zisizo kandamizi na adui kea Maendeleo na Uhuru.

 

Sheria na Kanuni sa sasa zinafanya SANAA NA UBUNIFU KUWA UHALIFU. Sio Sawa na Mimi binafsi sitakubali ibaki hivyo. Wizara iingilie Kati na Waziri (although I was critical of him) amebainisha kuleta mabadiliko na tunamtegemea aanze na hili. Bunge liingilie Kati, kea Kutunga upya sheria na kufuta hizi zilizo kandamizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *