Waogeleaji wa Uingereza, Sascha Kindred, Ellie Simmonds na Susie Rodgers wameshinda medali za dhahabu katika michuano ya kuogelea ikiwa ni siku ya tano ya michuano ya Rio Paralimpiki.

Kindred na Simmonds wote waliweza kuvuka rekodi mita 50 na kuvunja rekodi ya dunia.

Hii inaifanya Uingereza kushinda jumla ya medali 63, ambapo 28 kati ya hizo zikiwa ni medali za dhahabu.

Kindred mwenye miaka 38 alimaliza kwa saa 2:38:47 na kujihakikishia ushindi wake wa saba wa dhahabu katika michuano ya Paralimpiki kabla Simmonds mwenye miaka 21 kutetea taji lake kwa kutumia saa 2:59.81

Will Bayley na Aled Davies mapema kabisa walijinyakulia medali za dhahabu kwa timu yao ya Uingereza katika michuano ya tennis pamoja na mitupo ya mbali.

Kumekuwa na mafanikio katika timu za Uingereza mbapo John Stubs na Jodie Grinman walishinda medali ya fedha, kabla ya Waingereza wengine Sascha Kindred, Ellie Simmonds na Susie Rodgers kujishindia medali za dhahabu katika michuano ya kuogelea.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *