Mamia ya wahamiaji wasiokuwa na nyaraka za kubaki Marekani, wamekamatwa nchini humo katika siku chache zilizopita.

Maafisa wa uhamiaji walifanya msako katika miji ya Los Angeles, Atlanta, Chicago, New York, Texas na Carolina Kaskazini katika hatua za kufuata sheria chini ya serikali mpya ya Rais Trump.

Lakini wakuu wanasema misako hiyo ni ya kawaida, ya kuwakamata wahamiaji wahalifu na kuwaondosha nchini.

Wanasema hatua kama hizo zilikuwa zikifanywa wakati wa serikali zilizopita na siyo agizo la Trump kama wanavyodaiwa.

Shirika la kutetea haki za wahamiaji la Los Angeles, limesema mahabusu hawaruhusiwi kuwaona mawakili.

Serikali ya Mexico, ilionya raia wake walioko Marekani, wawe na tahadhari, na wawasiliane na ubalozi wao, baada ya mwanamke mmoja kutoka Mexico kuondoshwa kwa lazima siku ya Alkhamisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *