Wafanyabiashara 100 wa Jijini Dar es Salaam jana wameandamana ofisi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ili kujua hatima ya leseni zao za kusafirisha viumbe hai nje ya nchi.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Enock Balilemwa amesema wamefikia hatua hiyo baada ya Serikali kushindwa kuwapa majibu ya msingi juu ya kusitishwa kwa leseni zao.

Amesema kilio chao kinatokana na zuio la Serikali kupitia wizara hiyo ambapo tangu Machi 17, mwaka huu wamewaingiza kwenye hasara ambayo kwa sasa hawawezi kuimudu.

Mwenyekiti huyo alisema leseni hizo ambazo waliomba na kusitishwa zina madaraja tofauti ambayo yanaruhusu kukamata wanyama hao.

Mwenyekiti huyo alisema daraja jinigine ni la 16 ambalo linaruhusu kukamata mijusi na nyoka na daraja la 21 huwaruhusu kukamata wadudu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa wizara hiyo, Doreen Makayo, baada ya kusikiliza madai ya wafanyabiashara hao aliwaahidi kuwasiliana na Waziri Maghembe ili kujua hatima yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *