Jeshi la polisi nchini limewaka wafanyabiashara na wananchi wanaofanya manunuzi au kuuza bidhaa kwa njia za mtandao kuwa makini na matapeli wanaotumia mitandao kufanya uhalifu.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba na kutoa tahadhari hiyo kutokana na kuwepo kwa matukio mengi ya watu kuibiwa fedha zao wakati wa kuuza au kununua bidhaa kwa kutumia mitandao.

Bi Bulimba amesema kuwa  watu wamekuwa wakifanya biashara kwa njia za mtandao na matokeo yake wanajikuta wanaingia kwenye kutapeliwa kwenye kuibiwa kwasababu tu ametuma pesa kwa mtu ambaye hamfahamu, amefanya biashara na mtu ambaye hamfahamu yani wamewasiliana tu kupitia mtandao.

Pia amesema kuwa “Kwamba mimi nafanya biashara mbili tatu, mimi nauza kitu fulani nitumie pesa kiasi fulani ntakutumia mzigo, tunaomba wananchi wawe makini na hili suala kwasababu tumepokea matokeo mengi ya wananchi kutapeliwa kwa njia ya mtandao”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *