Timu ya taiafa ya Cameroon imepatwa na majanga baada ya wachezaji wake saba kugoma kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika Januari mwakani nchini Gabon.

Sababu za wachezaji hao kugoma ni kutokana na kuhitajika zaidi kwenye klabu zao mwezi huo wa Januari hivyo wameelekeza nguvu zao kwenye maslai binafsi kuliko taifa.

Pia inaelezwa uhenda kukawa na mgogoro kati ya wachezaji na shirikisho la mpira nchini Cameroon kutokana na kutopewa posho kipindi wanavyoitumikia timu hiyo taifa.

Ikumbwe kuwa Shirikisho la soka nchini Cameroon limeshawahi kuwa na mgogoro na wachezaji wake kwa kutowalipa posho mpaka kupelekea wachezaji kugoma katika mashindano makubwa kama kombe la dunia.

Nyota hao saba wasiotaka kuwa sehemu ya kikosi ni pamoja na beki mahiri wa Liverpool Joel Matip, Allan Nyom, anayechezea timu ya West Bromwich Albion, Andre Onana wa Ajax Amsterdam, Guy N’dy Assembe wa Nancy, Maxime Poundje anayechezea Girondins Bordeaux , Andre-Frank Zambo Anguissa wa Olympique Marseille pamoja na Ibrahim Amadou anayekipiga na Lille

 Kocha wa Cameroon Hugo Broos amesema wachezaji wameweka maslahi yao binafsi juu ya yale ya timu ya taifa hivyo shirikisho la soka la nchi hiyo linatakiwa kuchukua hatua kwa wachezaji hao kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *