Wabunge wa upinzani wametoka Bungeni leo mjini Dodoma kufuatia kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtoa nje ya Bunge, mbunge wa Kibamba, John Mnyika kutokana na utovu wa nidhamu.

Spika wa Bunge aliamuru mbunge huyo kutolewa nje ya bunge na kusema hataruhusiwa kushiriki katika vikao vya bunge kwa wiki nzima, jambo ambalo limepelekea wabunge wa upinzani wote kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga kitendo hicho.

Akizungumza nje ya bunge Mbunge Ester Bulaya amesema kuwa kazi ya wabunge wa upinzani ni kuishauri serikali, hivyo wao hawawezi kuishauri serikali vile ambavyo inataka kushauriwa.

Bulaya amesema kuwa wapo wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wamekuwa wakitumia lugha isiyo na staha lakini wamekuwa wakiachwa huku wabunge wa upinzani wakichukuliwa hatua kama hizo.

Pia Bulaya ameongeza kwa kusema kuwa wao kama Kambi ya Upinzani wameamua kutoka nje ya bunge kwa sababu hawawezi kujadili mambo ya msingi kwa kufanyiwa mambo hayo kwasababu kazi yao ni kuishauri serikali lakini hawawezi kuishauri serikali vile wanavyotaka wao.

Bulaya aliongeza kwa kusema kuwa kwenye Wizara ya Ardhi mbona wabunge wa upinzani walisimama na wakapongeza na Wizara ya Ardhi ilipita bila shida yoyote kwa pande zote mbili, sasa kwanini wao wanataka kupongezwa tu.

Alimaliza kwa kusema kazi yetu ni kuona pale ambapo mambo hayaendi sawa kwa mujibu wa sheria tunasema na hili liwe wazi watu waliokuwa wakipigia kelele mikataba mibovu ni upinzani bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *