Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya mandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na serikali ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania.
Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari la teksi nje ya bweni la chuo kikuu.
Maafisa wa shirika hilo wameandamana kwa pamoja nabaadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni kwa jina Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo aligongwa na kuuawa.
Yalikua maandamano salama na watu walikusanyika kwenye uzio wa seng’enge pahala gari lilipo mgonga marhem Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.
Mshukiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana.
Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.
Mkuu wa Africa Diaspora Forum Marc Bafou ameitaka serikali ya Afrika Kusini na serikali ya TZ pamoja na wakuu wa chuo kikuu cha Johannesburg mauaji haya wayape kipao mbele maana yatazidi kukiaibisha chuo kikuu cha Johannesburg na taifa la Afrika Kusini, mauaji yalioonekana kama chuki dhidi ya raia wa kigeni.
Africa Diaspora Forum imesema Tanzania inafahamu fika gharama ya kumpata mwanafunzi mmoja aliyehitimu shahada ya udaktari kwa hivo serikali ya Tanzania isiliachie suala hili kwa wepesi.