Vodacom imesitisha huduma za kununua Luku kwa wateja wa M-Pesa nchini kufuatia kutokidhi masharti ya mfumo wa malipo Serikalini(GePG).
Wamedai huduma hii itarejea pale makubaliano kati yao na Serikali yatakapokamilika juu ya mfumo huo mpya.
Zamani mawakala wote walikuwa wanapitia TANESCO lakini sasa wanatakiwa kujiunga na mfumo wa Serikali, hivyo mkataba unafanywa baina ya wakala na Serikali.
Kwa sasa, Kampuni za Tigo, TTCL na Airtel zimekidhi vigezo na kukamilisha utaratibu. Kampuni za Halotel na Zantel pia zinatarajiwa kujiunga kwenye mfumo huo.
Hata hivyo inadaiwa asilimia za malipo kwa mawakala zitapungua chini ya mfumo huo mpya unaonza kutumiwa na makampuni hayo.