Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wamemmjia juu mwanamuziki Diamond kutokana na kuimba wimbo ‘Hallelujah’ pamoja na kuvaa cheni za msalama kwenye video zake.
Mmoja wa sheikh hao, Sheikh Kipozeo amesema kuwa Diamond hajafanya vizuri kuimba wimbo huo kwa sababu huku ni kama kukiuka imani yake ya dini ya kiislamu na kumsujudia nabii Issa.
Sheikh Kipozeoa amesema kuwa Kitendo cha kuvaaa msalaba kilichoonyeshwa na Diamondni ishara ya yeye kuonyesha kuwa anakubali kuwa nabii issa kasulubiwa, sasa si bora hatuambie kuwa yeye sio muislamu, kwanini uwaambie watu kuwa wewe ni muislamu alafu unavaaa msalaba, na katika nyimbo zake si bora angeimba nimbo nyinyine nyingine tu, anaimba Halleluyah”.
Halleluyah ni moja ya nyimbo mpya za Diamond ambazo zinafanya vizuri duniani kote, wimbo huo uliotoka mwezi uliopita amewashirikisha kundi la muziki la MorganHeritage.
Ikiwa kama nyimbo mojawapo iliyomfanya Diamond aendele kujulikana kimataifa na anaona alipiga hatua kubwa katika muziki kutokana na kushirikiana na wanamuziki wakubwa Duniani, Diamond aliimba wimbo huo kwa dhumuni la kikidhi mahitaji ya mashabiki.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa msanii Diamond na wasanii wengine kuongelewa na viongozi wa dini zao kutokana na nyimbo wanazoimba, lakini kwa upande wa Diamond haijawa wazi kuwa mambo hayo yote ambayo Diamond amefanya katika wimbo huo alimaanisha kile ambacho viongozi wa dini watakuwa wamekimahanisha pia.
Bado diamond hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo alizoshtakiwa na viongozi wa dini yake, lakini nadhani inampasa kujibu ili aweze kuweka wazi kwa watu pia.