Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) wamefika leo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Sentro) kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Viongozi hao waliowasili ni Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika (Mb), Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche; Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) Halima Mdee ambaye alidai amewasindikiza wenzake na Ester Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.
Mnyika alisema hawakuhojiwa na badala yake wameambiwa warudi tena kituoni hapo Alhamisi ijayo, Feb. 27, saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa.
Pia Mnyika amesema viongozi wengine hawakuweza kufika kwa sababu wapo mbali na Dar huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Mashinji akiwa safarini nchini Marekani.
Wengine walioitwa lakini hawakupata nafasi ya kufika leo ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.