Hatimaye Umoja wa Afrika (AU) umefikia makubaliano ya kuirudisha nchi ya Moroko kwenye uanachama wa Umoja huo.
Moroko ambayo ilijitoa kwenye uanachama wa Umoja huo mwaka 1984 baada ya AU kuutambua uhuru wa Sahara Magharibi eneo ambalo Moroko ilikuwa inadai ni sehemu ya nchi yake.
Kwa kipindi cha miaka zaidi ya thelathini Moroko iliendelea kuw anchi pekee barani Afrika ambayo sio mwanachama wa AU.
Uamuzi wa kuirudishia uanachama nchi hiyo umefuatia juhudi zake za muda mrefu za kuomba kurejeshwa tena kwenye Umoja huo huku viongozi wan chi za Afrika wakipiga kura ya kuikubalia ombi hilo kwenye kikao cha AU kilichofanyika jana.
Sambamba na jambo hilo kubwa pia viongozi wa AU walimchagua waziri wa mambo ya nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat kushika wadhifa wa ukuu wa Tume ya Umoja wa Afrika akirithi mikoba ya Nkosazana Dlamini-Zuma.
Bw. Moussa Faki Mahamat alimshinda mpinzani wake, mwanadiplomasia wa juu wa Kenya, Amina Mohamed.