Mzee Willy Kinyua (98) amefunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.
Wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya.
Wanandoa hao wenye watoto watano wanatembea kwa kutumia fimbo kwasasa kutokana na uzee wao walionao.
Kinyua amesema, alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti.
Baada ya ndoa huyo Mzee huyo amesema kuwa “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti’.
Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake kama ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo.
Bibi hiyo amesema, alimpenda sana Kinyua na kwamba wamekuwa wakiishi kwa amani.
Kwa mujibu wa Nyambura, ndoa zinavunjika kwa sababu wanaume wengi wanawasaliti wake zao kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine.