Mamlaka ya Kuzuia na Kupamabana na Dawa za Kulevya imesema kuwa inawashikilia na kuwahoji vigogo watano waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wanaojihushisha na biashara haramu ya dawa z akulevya.
Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema kuwa wanawahoji na kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kabla ya kufikishwa mahakamani.
Kamishna huyo amesema majina hayo ya watuhumiwa hao wanatoka miongoni mwa majina 97 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyomkabidhi Kamishna Mkuu, Rogers Sianga Februari 13 mwaka huu.
Kuhusu kuwataja, Kamishna Kibula alisema muda muafaka ukifika watawataja ili wananchi waweze kuwafahamu.
Kuhusu majina ya watuhumiwa wengine 92, Kamishna Kibula alieleza kuwa wamekuwa wakiyafanyia kazi na kwamba hawakamati mtu hovyo, ni lazima wajiridhishe kuwa mtu huyu anastahili kukamatwa ndipo wafanye hivyo, lakini pia hawatangazi majina yao hadharani.
Kwa upande wake Kamishna Sianga amesema kuwa robo tatu (asilimia 78) ya wanawake wanaotumia dawa za kulevya ni waathirika wa UKIMWI kwa sababu ili kupata fedha za kununua dawa hizo hulazimika kufanya ngono zembe na hivyo kupelekea maambukizo ya UKIMWI kuzidi kupanda.