Idadi ya wakimbizi na wahudumu wa misaada ya binadamu waliofariki baada ya kushambuliwa kwa bahati mbaya na majeshi ya Nigeria kwa kudhaniwa ni Boko Haram imeongezeka.

Tukio hilo lililotokea wiki iliyopita kwenye eneo la Rann sasa limefikisha idadi ya watu waliofariki kuwa 115 baada ya jeshi la Nigeria kudhani kambi iliyokuwa ikihudumia wakimbizi kwenye eneo hilo ni ngome ya Boko Haram.

Kambi hiyo ambayo ilikuwa ikihifadhi na kuhudumia watu waliokimbia mauaji yanayosababishwa na wapiganaji wa kundi hilo ilijikuta ikipokea kipigo kutoka kwa jeshio la anga la Nigeria baada yakudhaniwa kuwa ni maficho ya wapiganaji wa Boko Haram.

Kosa hilo la kiufundi linadaiwa kuwa kubwa zaidi na lililosababisha madhara kwa watu wengi zaidi tangu kuanza kwa mapambano dhidi ya kundi hilo mwaka 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *