Mwanamitindo wa Marekani, Black Chyna amekumbwa na kashfa kubwa baada ya mkanda wa ngono alioshiriki kuvuja mtandaoni.
Video hiyo ilivuja kupitia mtandao wa Twitter umemuonyesha sura ya mrembo huyo akiwa na mvulani ambaye hadi sasa hajukani alikuwa nani kwasababu si mtu maarufu.
Video hiyo ilikuwa na muda wa dakika 1 na sekunde 23 ilimuonesha mwanamitindo huyo akiwa utupu wakati akishiriki video hiyo.
Baada ya kutokea hali hiyo Mwanasheria wa mrembo huyo Lisa Bloom alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji kwa mteja wake.
Mwaka 2017 Chyna aliingia katika ugomvi na mzazi mwenzake Rob Kardashian baada ya kuziachia picha zake za utupu mtandaoni.
Hadi sasa mwanamitindo huyo bado ajaongea chochote kuhusu hali hiyo iliyomchafua kutokana na kusambaa kwa video hiyo mtandaoni.