Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Snoop Dogg ametakiwa kuomba radhi baada ya kuachia video ‘Lavender’ akiwa amemuoneshea bastola Rais wa Marekani, Donald Trump.

Mwanasheria wa rais wa Rais, Michael Cohen ametoa taarifa hiyo ya kuomba msamaha kwa mwanamuziki huyo kutokana na kumkashifu Rais Trump.

Michael Cohen amesema kwamba kitendo ambacho amekifanya Snoop Dogg ni udhalilishaji kwa Rais Donald Trump na kusisitiza kwamba Snoop anapaswa kuomba msamaha kwa kitendo chake hicho.

Ni sawa kufanya utani lakini kwa upande wa Snoop Dogg amevuka mipaka ya utani kwa kile kikubwa ambacho alikifanya cha kutoa pisto ya uongo na kuinyoosha kwa mfano huo wa Donald Trump.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *