Mchezaji wa Chelsea, Victor Moses anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace ambapo walifungwa 2-1.
Mchezaji anaungana na Alvaro Morata na Ng’olo Kante katika orodha ya majeruhi wa Chelsea.
Moses atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne ambazo ni sawa na mwezi mmoja hali itakayompelekea kukosa mchezo kati ya Chelsea na Manchester United ambao utapigwa tarehe 5 mwezi ujao.
Moses atakosa jumla ya michezo saba ikiwemo mchezo wa Champions League dhidi ya As Roma na pia Bournemouth, Watford, Everton,Manchester United na West Bromich Albion.
Habari hizi zinaweza kuwa njema kwa mchezaji mpya wa Chelsea David Zapaccosta kwani anaonekana anaweza kuwa mtu sahihi kuziba pengo la Victor Moses ambaye msimu huu ulianza vizuri kwake.
Wakati huo huo Chelsea watakuwa uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge siku ya Jumatano ambapo wataikaribisha As Roma katika muendelezo wa michuano ya Champions League.