Papa Francis amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye makazi ya Papa Francis yaliyoko jijini Vatican.
Kwenye mazungumzo hayo Rais Kabila amesema atahakikisha anafanikisha mazungumzo ya pande zote zinazokinzana nchini Congo yamalizike kwa amani.
Kwenye mazungumzo hayo yaliyochukua dakika 20, Papa Francis hakwenda kusalimiana na mgeni wake huyo kwenye chumba maalum cha wageni maalum na kumsubiri kwenye maktaba yake.
- Vatican wamesema Papa Francis amesisitiza ni lazima mazungumzo ya amani yafanyike baina ya serikali na wapinzani ili kuliepusha taifa hilo kuingia kwenye machafuko.