Aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amethibitisha kuwa anatarajia mtoto wa pili na mpenzi wake Rotimi kutokana nchini Marekani.

Ni mwaka mmoja tangu Vanessa na mpenzi wake kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Nigeria, Rotimi kupata mtoto wa kwanza ambaye anaitwa Seven.

Kupitia Instagram ya Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa wapo karibuni kupata mtoto wa pili na mpenzi wake huyo.

Vanessa Mdee amesema kuwa tayari ana ujauzito wa mtoto wa pili na ni mtoto wake huyo atakuwa ni mtoto wa kike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *