Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amesema kwamba Joh Makini moja ya watu waliomtia faraja wakati alipokamatwa mwezi wa tatu na kukaa kituo cha Polisi kutokana na tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

Vanessa amesema kuwa Joh Makini alikuwa naye pamoja nyakati za usiku akimtembelea na kuhakikisha hakati tamaa wakati wa kipindi hiko kigumua.

Vanessa amefunguka na kusema kwamba hata baada ya kutoka kituo cha Polisi aliusikia wimbo wa Pumzi ya Mwisho uliofanywa   studio na alivutiwa na na ujumbe uliokuwepo kwenye wimbo huo.

Amesema kuwa “Kuna baadhi ya meseji sikuwahi kufikiria kuziweka kwenye Albamu yangu.  Pumzi ya Mwisho ni wimbo ambao sikuwahi kufikiria kuwepo kwenye Albam yangu ila baada ya kupitia changamoto za kukaa kituo cha polisi kwa siku kadhaa ilibidi meseji hii pia niiweke kwenye wimbo huu ambao nimeshirikiana na Johmakini pamoja na Casper Nyovest”.

Pia ameongeza kwamba; “Nisamehe Joh nakuuza lakini naombeni niseme kwamba Johmakini, Juma Jux pamoja na Ben pol ni watu waliokuwa kila siku wanakuja kituoni na kunitia moyo. Namshukuru sana na naweza kusema kwamba ndoto yang katika maisha ya muziki ilikuwa ni ndoto yuangu ya  kufanya kazi na msanii Johmakini”.

Mbali na hayo Vanessa Mdee amekiri kwamba albamu yake isingekamilika bila mpezi wake Jux kuwepo karibu kwani ni mtu ambaye alikuwa akimsukuma kuitoa kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *