Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na Mchekeshaji Idris Sultan ni miongoni mwa Watanzania waliofanikiwa kutajwa kwenye tuzo za mitindo nchini Nigeria za Nigeria Icons Fashion Awards – African Diaspora 2018.
Watanzania wengine waliotajwa kuwani tuzo hizo ni Wanamitindo Hamissa Mobetto, Sheria Ngowi, Ben Breaker, Richard George Maliti na Shawn Kieffer.
Vanessa Mdee ametajwa kwenye kipengele cha Most Stylish Female Artiste of the Year ambapo atapambana na Yemi Alade, Tiwa Savage, Nadia Nakai na Nsoki Neto.
Kwa upande wa Idris Sultan yeye atachuana na Wanaijeria wanne kwenye kipengele cha Most Stylish/Dressed Celebrity of the Year (Male).
Upigaji wa kura wa tuzo hizo utaanza Aprili 10, 2018 ambapo utaratibu wa kupiga kura itatangazwa rasmi hapo baadaye.