Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amekanusha kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Jux licha kuonekana pamoja.

Vanessa amekanusha taarifa hiyo baada ya kuenea taarifa za wawili hao kurudiana baada ya kuonekana pamoja kila wakati jambo ambalo limesababisha mashabiki wao kuhoji je wawili hao wamerudiana?.

Vanessa amesema kuwa hawajarudiana ila kilichopo sasa ni urafiki wa kawaida na si wa kimapenzi hivyo kila mtu ana mambo yake.

Vee Money amesisitiza kuwa hawajarudiana bali kilichopo sasa ni urafiki tu kwasababu hawezi kuacha urafiki na mwanamuziki huyo.

Amesema kuwa “Kitu ambacho nyie hamjui Jux ni mshikaji wangu ni mtu ambaye tunapatana na kufanya kazi pamoja hata vitu vingi ambavyo ni nje ya sekta ya muziki Jux anasapoti, hatuwezi kuanza kugombana na sasa hivi, tunakuwa tunaharibu biashara”.

Vanessa na Jux walikuwa wapenzi na kipindi cha mahusiano yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu ambao ulitamba sana kutokana na ujumbe wa nyimbo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *