Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Pancras Uwoya maarufu zaidi kama Irene Uwoya amejibu juu ya mpango wake wa kuolewa tena baada ya kuvunjika kwa ndoa zake za awali.

Irene mwenye umri wa miaka 32, muandaaji wa filamu, mfanyabiashara na mama wa mtoto mmoja wa kiume ‘Chrish’, alijibu kuwa ikijaliwa hilo tena yuko tayari.

Uwoya alijibu hilo kuhusu mpango wa ndoa baada ya swali la shabiki kupitia mtandao wa Instagram huku isibainike yuko kwenye mahusiano na nani kwa sasa.

Aidha, Uwoya alishapitia ndoa mbili baada ya ile ya marehemu baba wa mtoto wake, Hamad Ndikumana na ya msanii Dogo Janja iliyovunjika mwaka 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *