Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amesema kuwa huu ni wakati wake wa kufurahia mafanikio huku akiwataadharisha wanaomuiga.
Uwoya anasema kuwa, huu mwezi ni wake wa kula bata mwanzo hadi mwisho hivyo asifuatiliwe wala asiigwe na baadhi ya watu.
Uwoya amesema kuwa, hii ni kwa sababu huu ndiyo mwezi wake wa mafanikio makubwa hivyo amejipangia kufurahi kwa kufanya ziara kubwakubwa ndani na nje ya Tanzania.
Uwoya amesema kuwa ana furaha mno na amepanga kuzunguka sehemu tofauti nchini kwa ajili ya kufurahi kwa sababu ana amani kubwa mno moyoni mwake.
Mama huyo wa mtoto mmoja anasema kuwa, amepanga akimaliza ziara ya hapa Bongo, basi ataenda kumalizia nchini Mexico ambako kuna viwanja vya bata vya kutisha.