Mwili wa kiongozi wa upinzani nchini DR Congo, Etienne Tshisekedi hautarudishwa nyumbani wiki hii kama ilivyopangwa.

Familia ya Bwana Tshisekedi aliyefariki mwezi uliopita nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84 alikuwa amepanga kufanya mazishi nchini DR Congo Jumamosi inayokuja.

Nduguye mdogo bwana Tshisekedi Gerard Mulumba aliambia amesema kuwa familia haijakukubaliana na serikali kuhusiana na eneo atakalozikwa marehemu mjini Kinshasa.

Familia ya Tshisekedi wanataka mwili uzikwe katika makao makuu ya chama cha UPDS alichanzisha.

Lakini serikali inataka kumzika katika makaburi ya Gombe yalioko katikati ya mji wa Kinshasa nchini humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *