Rais wa Marekani, Donald Trump utajiri wake umeshuka kwa nafasi 220 hadi kufikia nafasi 544 kwenye orodha iliyotolewa na Forbes.

Forbes wamesema kuwa utajiri wa Trump umeshuka kwa $1bn na sasa anamiliki mali ya $3.5bn pekee.

Kushuka kwa utajiri wa Rais huyo kulitokana na kuupungua kwa kasi ya sekta ya biashara ya ardhi na makao nchini Marekani.

Pia Jarida hilo pia limesema utajiri wake uliathiriwa pia na matumizi katika siasa, sana kwenye kampeni yake ya urais ambapo inakaribiwa alitumia $66m.

Aidha, alitumia $25m kumaliza kesi ambapo alishtakiwa kwa tuhuma za kuwatapeli wanafunzi kupitia Chuo Kikuu cha Trump.

Hata hivyo, Forbes wamesema thamani ya hoteli ya Mar-a-Lago jimbo la Florida ilipanda $25m kutokana na kuangaziwa sana baada ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *